Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) umeomba kuidhinishiwa tsh. bilioni 25.34 kwa ajili ya kununua vifaa vya maabara kwa shule mpya 234 za kata na kuendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa Elimu ya Sekondari na shughuli nyingine.
Hayo yameyasemwa Aprili 14, 2024 Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Akifafanua maombi ya fedha hizo zilizoombwa kuidhinishiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema ni pamoja na kununua vifaa vya maabara na kemikali kwa ajili ya shule mpya 234 za Sekondari za Kata zinazojengwa katika Halmashauri.
Waziri Kairuki ameongezea kwa sema fedha hizo pia zimepangwa kununua vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya shule 1,000 za sekondari za kata kwa ajili ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mradi katika maeneo ya ujenzi wa shule mpya za sekondari, kuwezesha utendaji kazi wa Ofisi ya Rais –TAMISEMI katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari.
Pia amesema zitasaidia kuwezesha utangazaji wa shughuli zinazotekelezwa na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa wananchi ili waweze kufahamu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha elimu ya sekondari nchini na kuwezesha kuwajengea uwezo watumishi 68 wa Idara ya Usimamizi wa Elimu katika masuala yahusuyo ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Aidha, Mhe.Kairuki baada ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2023/24 ameliomba Bunge kuridhia kuidhinishiwa sh. trilioni. 9.1 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
|
|
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa