Imeeleazwa kuwa jamii yoyote yenye utawala wa kisheria , watu lazima wawe na fursa ya kupata haki na waweze kutatua migogoro yao na kupata nafuu au tuzo mbalimbali zinazoendana na haki za binadamu kwa kupitia taasisi mbalimbali za utoaji haki zilizowekwa kisheria.
Hayo yamebainishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kilosa Timothy Lyon katika siku ya sheria nchini ambapo amesema kuwa mwaka 2019 siku ya sheria nchini inaongozwa na dhima isemayo utoaji haki kwa wakati: wajibu wa mahakama na wadau ambapo utoaji wa haki kwa wakati unaweza kuonekana bayana katika nchi endapo kila mdau mwenye wajibu katika utoaji wa haki atatimiza wajibu wake ipasavyo.
Akiongea katika siku hiyo Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa mahakama ni mahali ambapo wananchi wanategemea kuona haki ikitendeka hivyo ipo haja ya mahakimu katika mahakama zote kuwa watenda haki na wawe mstari wa mbele kuhakikisha haki inatendekea inavyostahiki ili kuondoa malalamiko ya wananchi dhidi ya mahakimu ambao wamelalamikiwa kwa vitendo vya kupokea rushwa.
Aidha Kasitila ambaye pia ni Katibu wa kamati ya maadili ya mahakimu amesema kamati yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kwamba imefika wakati wa kamati hiyo kuchukua sheria zinazostahili kwa mahakimu wote wanaolalamikiwa ili kujenga taswira nzuri baina ya wananchi na mahakimu na kwamba ifike wakati haki itendeke lakini pia kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa