Wasimamizi wa ngazi ya kata, watendaji na vijiji pamoja na waratibu elimu kata wametakiwa kusimama katika majukumu yao ipasavyo hususani katika matumizi ya rasilimali za umma jambo litakalosaidia rasilimali hizo kutumika ipasavyo huku wakitakiwa kuwa shirikishi kwa wananchi ili kuepusha migogoro na malalamiko toka kwa wananchi kutokana na usimamizi mbovu.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Rwegerela Katabaro ambapo amesema watendaji hao wanao wajibu wa kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao na kwamba wanao wajibu wa kuhakikisha changamoto hizo zinaisha ama kupungua.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya Dira Erasmo Tullo amesema Ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kusimamia kikamilifu rasilimali za umma jamii na viongozi wanapaswa kuwa na uwazi jambo linalosaidia kuwa na matokeo chanya kwani uwepo wa uwazi hupelekea jamii kuwa na ushiriki mzuri ambapo miongoni mwa mambo yanayopaswa kuwa wazi ni usomaji wa taarifa za mapato na matumizi , ufanyikaji wa mikutano stahiki katika vijiji na mashuleni na kubandika taarifa za mapato na matumizi maeneo husika.
Tullo amesema licha ya uwepo wa changamoto lakini pia katika kata ambako taasisi hii inashiriki katika kuhakikisha kunakuwa na usimamizi yapo mafanikio yaliyojitokeza ambayo yamebainishwa na watendaji wa kata za Tindiga, Kilangali, Mabwerebwere na Ulaya ikiwemo upatikanajni wa chakula mashuleni kwa baadhi ya shule, ujenzi wa vyumba vya madarasa upatikanaji wa walimu wa ziada wa kujitolea, baadhi ya maneno yamekuwa yakibandika taarifa katika ofisi za vijiji na mashuleni, ujenzi wa ofisi ya walimu na ujenzi wa matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa