Watendaji wa kata na vijiji wametakiwa kuhakikisha taarifa za mapato na matumizi zinatolewa kwa wananchi kila vinapofanyika vikao vya kisheria jambo litakalosaidia kufanikisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao ikiwemo ujenzi wa madarasa ambapo wamesisitizwa kuwafahamisha wananchi kinachopaswa kujengwa si boma bali ni darasa jambo litakalosaidia kutokuwa na maboma ambayo hayajamaliziwa kwa kuisubiri Serikali imalizie ujenzi.
Rai hiyo imetolewa Machi 18 mwaka huu na Mkaguzi wa Ndani Wilaya Eliuta Makugila ambapo amesema kumekuwa na maboma mengi ambayo hayajamaliziwa kwa kusubiri Serikali imalize ujenzi jambo ambalo si sahihi huku akisema kuwa ili shughuli za maendeleo ziende Halmashauri ya kijiji inapaswa kushirikisha jamii katika maamuzi ya aina mbalimbali kupitia mkutano mkuu wa kijiji na kwamba kutofanyika kwa mikutano stahiki ndio chanzo cha migogoro.
Bi Christina Hauli Afisa Elimu Msingi Wilaya
Bi Paula Nkane Afisa Elimu Sekondari Wilaya
Akizungumzia suala la walimu kutoishi katika nyumba zilizojengwa na vijiji kwa ajili ya walimu amesema walimu wanaofanya kazi katika kata zilizo karibu na Kilosa mjini wamekuwa na hulka ya kutopenda kuishi katika kata husika kwa hoja ya kutokuwepo nyumba za kuishi katika kata husika jambo ambalo si kweli na linalipelekea watumishi hao kuchelewa kazini na kutoanza majukumu kwa wakati hivyo kila mtumishi anapaswa kuishi katika eneo lake la kazi hivyo ametaka watumishi wote kutimiza wajibu wao katika muda stahiki.
Naye Kamanda wa TAKUKURU Wilaya Lawrance Mlaponi amesema miradi mingi inafanywa kutokana na michango ya wananchi hivyo ili wananchi waweze kuchangia shughuli za maendeleo ni lazima wapate taarifa sahihi za mapato na matumizi kwani ni haki yao na ndio wachangaji wakuu hivyo kutotolewa kwa taarifa ama michango inayokusanywa isiposimamiwa vizuri na kuliwa na baadhi ya viongozi kunawavunja moyo huku akisisitiza pesa yoyote inapopelekwa shuleni ni vema mwalimu mkuu ama mkuu wa shule akashirikisha viongozi wengine ili kuepuka kujihusisha katika vitendo vya kijinai na kupelekea kupoteza kazi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa