Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ameendelea kuzitaka taasisi mbalimbali kuiga mfano wa taasisi ya kiislam iliyotoa eneo lake kuwa kambi kwa ajili wagonjwa wa corona lakini pia ameishukuru hospitali ya St Kizito Mikumi kwa namna walivyoonyesha ushirikiano ambapo hospitali hiyo ilimpokea mgonjwa wa corona mwanaume mwenye umri wa miaka 23 kutoka kituo cha Afya Mikumi na kuweza kumhudumia vizuri ambaye kwa sasa anaendelea vizuri huku akiendelea kuzitaka taasisi nyinginezo kuwa sehemu ya ushirikiano katika kupambana na janga la ugonjwa wa corona.
Mgoyi amesema kuwa ushirikiano ulioonyeshwa na hospitali ya St. Kizito na taasisi ya kiislam iliyotoa jengo lake lililokuwa ni zahanati ya Sarataini ni jambo la kuigwa kwani janga la corona ni janga la kitaifa hivyo ni vema taasisi zote zikaunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha jamii inakuwa salama kwa kuchangia vifaa mbalimbali ili jamii iweze kujikinga na janga hilo.
Aidha Mgoyi amewata viongozi wa kata, vijiji, mitaa na vitongoji kuendelea kuwafatilia wananchi wanaowaongoza na kuwa kipaumbele kuungana na wataalam wa afya hususani katika familia ambazo zina wahisiwa wa ugonjwa wa corona kwani madaktari waliopo ni wachache na kazi iliyopo katika kuhakikisha maambukizi hayaendelei ni kubwa na inayohitaji ushirikiano wa hali ya juu toka kwa serikali, viongozi wa kata na vyombo vya usalama.
MGANGA MKUU DKT. GEORGE KASIBANTE AKITOA MAELEZO NAMNA JENGO LA SARATAINI LITAVYOTUMIKA KWA AJILI YA WAGONJWA WA CORONA
Pamoja na hayo Mgoyi ametaka viongozi mbalimbali katika maeneo yao pamoja na Jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa corona kwani bado jamii inauhitaji wa elimu lakini pia kuhakikisha vikao vya kisheria vinafanyika ipasavyo lengo ikiwa ni kiuhakikisha hatua stahiki zinafuatwa ili jamii iwe salama.
DKT. LUCY WA HOSPITALI YA WILAYA YA KILOSA AKIUELEKEZA MSAFARA WA MKUU WA WILAYA KWENYE JENGO AMBALO LITATUMIKA KWA AJILI YA KUWAHUDUMIA WAGONJWA WA CORONA JENGO HILO LILILO CHINI YA TAASISI YA KIISLAM LINAJULIKANA KAMA ZAHANATI YA SARATAINI LIPO MIKUMI.
Aidha ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na kuzingatia taratibu stahiki zinazoelekezwa na wataalam wa afya lakini pia akitaka kutokuwepo kwa taharuki bali kuendelea kujikinga na kwamba katika shughuli za utafutaji riziki wahahakishe wanachukua tahadhari zote ikiwemo uvaaji barakoa, matumizi ya vitakasa mikono na unawaji mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.
SISTA ANTUSA MARIA WA HOSPITALI YA ST. KIZITO AKITOA MAELEZO NAMNA WALIVYOMPOKEA MGONJWA NA USHIRIKIANO ALIOUPATA TOKA WILAYANI
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mt. Kizito St. Antusa Maria Francis ameushukuru uongozi wa Wilaya ya Kilosa kwa namna ilivyoonyesha ushirikiano baada ya kubainika kwa mgonjwa huyo ambapo ametaka ushirikiano huo kuendelea kuwepo kwani kwa kupitia umoja huo tunaweza kufanikisha kuudhubiti ugonjwa wa corona na jamii kuwa salama huku msimamizi wa taasisi ya kiislam kwa upande wa Kilosa ambaye pia ni msimamizi wa jengo la Sarataini Abubakari Mhagama amesema uongozi wa Islamic Foundation umetii wito wa Serikali na Wilaya kiujumla kwa kutoa jengo lao liweze kutumika kwa kwa ajili ya janga la corona kwani ni jango lisilochagua jamii fulani bali mtu yoyote anaweza patwa na ugonjwa huo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa