Wakuu wa idara 20 wa Halmshauri ya Wilaya ya Kilosa Mei 07, 2018 wamejengewa uelewa wa pamoja juu ya utaratibu wa kutekeleza shughuli za Kuweka Akiba na Kukuza Uchumi wa Kaya Maskini ikiwa ni mpango unaotekelezwa na TASAF katika awamu ya tatu ikiwa ni sehemu ya Mpango Mkuu wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Hayo yamebainishwa na Afisa Utumishi Wilaya ya Kilosa Noel Abel kwa niaba ya mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ambapo amesema kuwa shabaha kubwa ya mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa pamoja katika ngazi zote za utekelezaji katika Halmashauri kwa kutoa mafunzo elekezi kwa watendaji husika ili kuwasaidia walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini ili waweze kushiriki katika shughuli za kukuza uchumi wa kaya
Mpango wa Kukuza Uchumi wa Kaya unahusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali ambazo zitasaidia ukuaji wa uchumi wa kaya ambapo shughuli hizo zinahusu uhamasishaji wa walengwa wa vikundi kuweka akiba ambazo zitatumika kama mitaji ya kuanzisha au kupanua shughuli za kiuchumi huku ikitarajiwa kuwa walengwa kupata ujuzi utakaowasaidia kutekeleza miradi au biashara kwa faida endelevu, hivyo kuongeza kipato na kupunguza umaskini
Awali Abel amesema kuwa TASAF imekuwa ikifanya kazi katika awamu mbili tofauti ambapo awamu ya kwanza miradi 1,704 yenye thamani ya shilingi bilioni 72 ilitekelzwa huku awamu ya pili miradi 12,374 yenye thamani ya shilingili bilioni 430 za kitanzania ilitekelezwa na kuwezesha jumla ya kupata huduma bora za kijamii ikiwemo huduma za afya,elimu , maji nk
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa