Taasisi, mashirika na wadau mbalimbali wameendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na ugonjwa wa corona kwa kutoa vifaa mbalimbali lengo ikiwa ni kuhakikisha wakazi wa Kilosa wanakuwa salama na kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Mei 29 mwaka huu shirika la TAZAMA PIPE LINE limekuwa moja ya wadau waliounga mkono wito uliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kwa kutoa vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Francis Kaunda kisha kukabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Wilaya.
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja Rasilimali Watu TAZAMA PIPE LINE Deogratius Msemwa ambapo amesema TAZAMA iko pamoja na watanzania katika kupambana na janga la corona ambapo imekuwa ikigawa vifaa mbalimbali katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo katika Wilaya ya Kilosa imekabidhi ndoo za gia za kunawia mikono 8, vipima joto kwa mbali 4, sabuni za kunawia mikono katoni 2, barakoa boksi 4 na gloves boksi 10.
Akishukuru kwa niaba ya Mkurugenzi Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. George Kasibante amesema kama msimamizi wa afya anashukuru kwa vifaa hivyo kwani vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwalinda watumishi na wagonjwa wanaopatikana kwani vitawasaidia kuhakikisha usalama wa wagonjwa na wahudumu wanapokuwa katika vituo vya kutolea huduma.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa