Timu ya Wataamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mkoa imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 5.3 inayotekelezwa Wilayani Kilosa.
Ziara hiyo imefanyika Julai 15, 2025 ikiongozwa Afisa Mipango Mkuu kitengo cha ufuatiliaji na Tathmini TAMISEMI Ndg. Henry R. Mutungo ambapo amesema ziara hiyo imelenga kufanya ufatiliaji wa Miradi ya Elimu Msingi, Sekondari na Majengo ya Utawala kisha kufanya tathimni ya utekelezaji.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mutungo amewataka wahandisi wanaosimamia miradi kuhakikisha wanafanya tathmini ya mradi kwa usahihi kulingana na maeneo husika ili kupata kiwango cha bajeti cha uwakika kitakachoweza kukamilisha miradi.
“Wahandisi fanyeni tathimini ya majengo kwa uwakika kulingana na eneo ambao mradi unatekelezwa ili kupata bajeti itayoweza kukamilisha mradi”. Alisema Mutungo
Aidha, ameongeza kuwa wasimamizi wa Miradi hiyo kuongeza juhudi ya usimamizi kwa kutoa ushirikiano na kufatialia kwa kila hatua ya ujenzi ili kuepuka changamoto zinazorekebishika wakati wa utekelezaji wa mradi.
Pia timu hiyo imeshauri kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi na Ugavi kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya mfumo wa Nest kwa mafundi ili waweze kupata uelewa wa kuomba zabuni ili kutatua changamoto ya uchache wa mafundi wanaoomba zabuni hizo hali inayopelekea miradi kutokamilika kwa wakati.
Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Mkoa Bi. Edina Katalaiya ameutaka uongozi wa shule kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya utunzaji wa miundombinu ili miradi iweze kutumika kwa muda mrefu huku akisisitiza suala la utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bi. Beatrice Mwinuka amesema amepokea maoni na ushauri mbalimbali yaliyotolewa na timu hiyo juu ya ukamilishaji wa miradi hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi.
Katika ziara hiyo miradi iliyotembelewa ni Pamoja na Jengo la Utawala , Nyumba ya Mkuu wa idara, Shule ya Msingi Matongolo, shule ya Sekondari Amali, Dumila na Chanzuru.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa