Wito umetolewa kwa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba kutumia vema mafunzo waliyojifunza ili kukuza ulinzi na usalama kwa kutetea na kulinda rasilimali za taifa hasa katika kukemea utoaji na upokeaji rushwa sambamba na uingizwaji wa mifugo kiholela jambo ambalo limekuwa likisababisha migogoro wilayani Kilosa.
Wito huo umetolewa katika kata ya Ulaya na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa wahitimu 48 wakiwemo wanawake 7 na wanaume 41 ambapo amesema kuwa mafunzo hayo yanawasaidia vijana kwenye suala zima la ajira na kupewa kipaumbele wakati wa kujiunga na Jeshi la Ulinzi Tanzania.
Naye Mshauri wa Jeshi Luteni Kanali Makyao amewataka wanaohusika na usaili wa mafunzo ya Jeshi la Akiba kufanya sensa ili kujua wahitimu wote na kuwapatia vitambulisho au vithibitisho ili kuzuia uhalifu unaotokana na kughushi nyaraka hizo na kuharibu uhalisia wa jeshi hilo
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa