Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ametoa rai kwa wananchi kupendelea kupata matibabu katika zahanati zilizopo katika maneneo yao ya karibu kwani huduma za kitabibu zinapatikana halikadhalika dawa muhimu zinapatikana katika zahanati hizo.
Mgoyi amesema changamoto zilizokuwa zikikabili zahahani zilizopo katika vijiji zimeshatatuliwa ambapo amesema changamoto kubwa ilikuwa ni uhaba wa matibabu na vifaa tiba ambapo kwa sasa serikali imekuwa ikifanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.
Aidha Mgoyi amewataka watendaji wa kata zote wilayani Kilosa kutambua vyema hatua kwa hatua huduma ya mfuko wa afya ya CHF na taratibu zake ili kutoa elimu kwa wananchi faida za mfuko huo, kisha kusimamia zoezi zima la uhamasishaji na uandikishaji wa kadi za huduma ya mfuko wa afya ya CHF, na kuhakikisha wananchi wote wanapata kadi hizo zitakazowasaidia katika upatikanaji wa huduma za afya.
Mgoyi ameongeza kusema kuwa serikali imetoa mwongozo kwamba kuanzia tarehe 01/07/2018 upatikanaji wa kadi za CHF zitapatikana kwa shilingi 30,000 kwa kaya ya watu sita badala ya shilingi 10,000 inayotumika kwa sasa kwa kaya ya watu sita, hivyo amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ya kupata kadi jambo ambalo litawasaidia kupata huduma za kitabibu na dawa kwa gharama nafuu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa