Serikali ya Switzerland imeendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kupunguza madhara yatokanayo na mabadikliko ya tabia kupitia program mbalimbali kwa vijana kufanya shughuli rafiki kwa mazingira ikiwemo upandaji miti ya kutosha ambayo itakuwa ikipandwa katika maeneo mbalimbali yatakayotengwa kwa ngazi ya vijiji.
Hayo yamebainishwa mwanzoni mwa wiki hii na Mkuu wa Sehemu ya Ajira na Mapato ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania Bw.Peter Sidler wakati wa uzinduzi wa kampeni ya vijana ya upanndaji miti ambapo amesema uwepo wa miti ya kutosha utasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia miti hiyo ya aina mbalimbali miti maji, mizambarau na mingineyo itasaida kupunguza athari za mafuriko lakini pia itasaidia shughuli mbalimbali ndani ya vijiji ikiwemo ujenzi wa ofisi za vijiji, upatikanaji wa samani mbalimbali ambazo zinaweza kutumika shuleni, vituo vya afya na zahanati
Mratibu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji Morogoro(MVIWAMORO) Joseph Sengasenga amesema kapitia kampeni ya youth green MVIWAMORO imetoa miche ya miti 5000 kwa kata za Rudewa kwa kijiji cha Rudewa Gongoni na Mvumi ambapo kila kata imepata miche ya miti 2500 ambayo inapandwa katika maeneo ya mikakati ikiwemo maeneo ya nyumba za ibada, ofisi za watendaji wa vijiji na kata, shule za msingi na sekondari, vituo vya afya na zahanati pamoja na maeneo ya taasisi zilizopo katika vijiji husika.
Sengasenga amesema pamoja na ugawaji wa miti pia wametoa elimu kwa vijana 50 juu ya utunzaji wa mazingira na ufundi stadi elimu ambayo itawasaidia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba kupitia upandaji miti ya aina mbalimbali itasaidia kutunza mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia vijana hao watapata miche ya miti ambayo watapanda maeneo malimbali kwa lengo la kujiongezea kipato kupitia miti ya mbao na matunda.
Kwa upande wake Afisa Mazingira Amal Shebe amesema upatikanaji wa miche ya miti 5000 kwa kata ya Rudewa na Mvumi itasaidia kwa kiasi kikubwa kupandwa kwenye kingo za maji hivyo kupelekea kupungua kwa adha ya mafuriko, kwani maeneo mengi ni hatarishi na hayafikiki kwa urahisi kwani kijiografia maeneo mengi ya Kilosa yapo chini hivyo kingo za maji zinashindwa kuhimili maji yanayotoka maeneo ya juu na kwamba Halmashauri inaendelea na jitihada za kupanda miti kwa wingi ili kuepuka madhara ya mafuriko.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa