Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kilosa na Mikumi Asajile Lucas Mwambambale amewataka wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata pamoja na waandikishaji wasaidizi watakaohusika katika zoezi ka uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura kuzingatia taratibu zote zinazoelekezwa na tume ya uchaguzi pamoja na kuzingatia taratibu za kujikinga na janga la corona kipindi chote cha zoezi hilo.
Mwambambale ametoa msisitizo huo Aprili 30 mwaka huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili ambapo amewataka washiriki hao kutambua kuwa wameaminiwa kushiriki zoezi hilo ambalo linafanyika nchi nzima ambapo katika wilaya ya Kilosa zoezi la uboreshwaji linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Mei 2 hadi 4 mwaka huu katika kata zote 40 ambazo kila kata itakuwa na kituo kimoja.
Pia amesema kuwa Tume ya uchaguzi katika zoezi hili la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura imeendelea kusisitiza namna ya kuchukua hatua madhubuti dhidi ya covid 19 ambayo huambukizwa kwa njia ya mgusano na njia ya hewa njia ambazo ni rahisi kuambukizana ikiwemo kwa kukohoa, kupiga chafya ama kugusa vitu mbalimbali vilivyoguswa na mtu mwenye maambukizi hivyo katika zoezi hilo wahakikishe vituoni hakuna msongamano, watu wanakuwa katika umbali wa kuanzia mita moja kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine, unawaji mikono kwa maji safi na salama na sabuni lakini pia amekumbusha watu kurejea tiba kinga za kale zilizotumika na wazee ikiwemo kujifukiza na kufanya mazoezi.
Licha ya hayo amesema Tume ya uchaguzi inaeleza kuwa zoezi la uboreshaji litawahusu watu wote ambapo litahusisha uwekaji wazi daftrai la kudumu ili watu waweze kuboresha taarifa zao huku ikisisitiza wasimamizi hao kuepusha misongamano katika vituo vyao pamoja na uwepo wa ndoo zenye maji safi na salama pamoja na vitakasa mikono ambapo pia katika vituo licha ya kuwepo kwa waandikishaji lakini pia watapaswa kunawa mikono wafikapo vituoni kabla ya kupata huduma.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa