Imeelezwa kuwa uboreshwaji wa usafi wa mazingira sambamba na uboreshaji wa afya ikiwemo unawaji mikono nyakati muhimu, matumizi ya kichanja majumbani pamoja na matumizi sahihi ya choo ni miongoni mwa mambo yanayoweza kusaidia kwa kiasi kubwa kupunguza magonjwa yatokanayo na uchafu wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mshauri wa Maji na Usafi wa Mazingira kutoka SAWA Mhandisi Wilhelmina Malima ambapo amesema kuwa SAWA NA WARIDI kwa kushirikiana na Halmashauri katika kuongeza nguvu ya kuboresha afya kupitia huduma za usafi wa mazingira ambapo watahakikisha katika kampeni hii ya kitaifa watahakikisha vijiji 40 visivyo na vyoo vinakuwa na vyoo bora.
Malima amesema kuwa katika program yao wamepanga mkakati wa kuhakikisha kuwa zinapatikana kaya nyingi zitakazokuwa na vyoo bora ili kuepuka kujisaidia porini sambamba na baadhi ya shule zitakazopangiwa mkakati wa kujengewa vyoo unaofadhiliwa na WARIDI ambapo watendaji wakuu wakiwa ni SAWA ambao watahakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
Naye Mratibu wa Usafi nau Mazingira katika program ya WARIDI Alex Ndama amesema ndani ya program hiyo inayokwenda kwa kaulimbiu usichukulie poa nyumba ni choo amesema licha ya kuhamasisha watu kujenga vyoo na kuvitumia , kuhamasisha unawaji mikono nyakati muhimu lakini pia watajenga vyoo katika shule mbalimbali za msingi za Madudu, Kitete, Mfulu na Peapea.
Naye Afisa Afya Nyabahwela Mahuyu amesema kuwa baada ya kufanyika kwa kampeni na uhamasishaji wa ujenzi wa vyoo hali halisi mpaka Disemba 2018 kaya 4048 zilikuwa hazina vyoo lakini kufikia Januari 2019 kaya 3050 katika ngazi ya wilaya ndio zilikuwa hazina vyoo ambapo kwa sasa takwimu zinaendelea kushuka kutokana na hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa kwa ngazi ya kata ikiwemo kupelekwa mahakamani kwa kaya zisizo na vyoo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa