Imeelezwa kuwa siku ya Maadili imezaliwa kutokana na Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ni siku maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuhimiza jamii kuzuia na kupambana na rushwa ambapo Serikali ya Tanzania iliamua kuwa maadhimisho hayo yafanyike Desemba 10 ya kila mwaka badala ya Desemba 9 kwa kuwa Tanzania huadhimisha sikukuu ya Uhuru ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu ni "Udhibiti wa mgongano wa maslahi: nguzo muhimu kujenga utawala bora"
Hayo yamebainishwa na Afisa wa TAKUKURU Lupakisyo Mwakyolile ambapo amesema kuwa hatua ya kusainiwa kwa mkataba wa Umoja wa mataifa wa kuzuia na kupambana na rushwa ilitokana na umoja wa mataifa kutambua kuwa rushwa si tatizo la taifa moja bali ni tatizo la dunia nzima na hivyo kuhimiza umuhimu wa nchi wanachama kushirikiana katika kuzuia na kupambana na rushwa duniani.
Lupakisyo amesema kuwa katika siku hii, jamii ya watanzania inapaswa kujitathmini imefanya nini, inafanya nini na itafanya nini ili kuimarisha, kuendeleza na kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa nchini, lengo ikiwa ni kuimarisha, kukuza na kusisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia maadili kama hatua muhimu katika kuzuia na kupambana na rushwa nchini, Serikali na wadau wote kutambua mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya rushwa nchini, Serikali na wadau wote kubainisha madhara ya rushwa na kutambua umuhimu wa kuendelea kuzuia na kupambana nayo,Serikali na wadau kutambua changamoto zinazokabili mapambano dhidi ya rushwa, Wadau wote kushiriki kuweka mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa na Tanzania kutathmini ushiriki wake katika mapambano dhidi ya rushwa kimataifa ikiwa ni hatua ya kuendeleza juhudi zake kujenga jamii inayoichukia na kuachana na rushwa.
Lupakisyo amesema maadili kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu ni mwenendo mwema wa mtu ambao unapimwa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miiko iliyokubalika na kuwekwa na jamii au kikundi cha watu ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa., ikiwemo kufuata kwa kanuni na watumishi wa umma ili utumishi wa umma uwe wenye ufanisi na unaoheshimika ikiwemo kutokuwa mbinafsi, Uadilifu, kutoa huduma bila upendeleo, kuwajibika kwa umma, uwazi na uaminifu
Ni wajibu wa kila mtanzania kudumisha uadilifu ili azma yetu, mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa tunayojiwekea ifanikiwe kwani suala la kutoa au kupokea rushwa huwa ni siri, lakini athari za tendo hili si siri kwani humgusa kila mwanajamii na athari ambazo kwa mujibu wa mapatano haya zinaathiri pia jamii na uchumi wa mataifa na sio wa nchi moja pekee.
Sambamba na hayo amesisitiza na kusema kuwa mgongano wa maslahi ni ishara ya hali hatarishi na inabidi idhibitiwe isimamimwe na kubainishwa kwa kuwa ina uwezo wa kuipa sifa mbaya serikali, sekta ya umma, idara na viongozi wasitumie ofisi zao kujinufaisha wao wenyewe ama ndugu zao, jamaa zao au wasishawishiwe na vitu hivyo kwa maslahi yao wenyewe saa zote ni maslahi ya umma na ya taifa ndio yanayosimama.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa