Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imewahakikishia wananchi juu ya upatikanaji wa Sukari Nchini ambapo tayari Shehena ya Bidhaa hiyo Tani 100,000 imeshaingia Nchini na kubainisha kuwa Sukari hiyo itauzwa kwa bei elekezi kati ya shilingi 2700 hadi 3200 kwa kilo.
Hayo yamebainishwa Januari 29,2024 na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde wakati wa Ziara ya Kamati ya Bunge ya Biashara,Viwanda,Kilimo na Mifugo ilipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kilichopo Wilayani hapa ambapo amekiri kuwepo kwa uhaba wa Sukari Nchini unaotokana na Viwanda kushindwa kuzalisha kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivyo kusababisha bei ya Sukari kupanda.
Mhe Silinde amesema kuwa Serikali ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan mpaka sasa imeshachukua hatua ya kudhibiti changamoto hiyo kwa kuagiza Tani laki moja za Sukari ambapo itauzwa kwa bei elekezi ili kila Mtanzania aweze kumudu na kusisitiza kuwa Meli tayari zimeshatua Bandarini na kwamba zipo kwenye maandalizi ya kushusha mzigo huo.
Aidha amesema kuwa Wizara imejiwekea mikakati ya Muda Mrefu na Muda mfupi na kwamba mkakati wa Muda mrefu ni Pamoja na kuondoa kabisa changamoto ya Uhaba wa Sukari Nchini kwa kuongeza uzalishaji katika Viwanda vya sukari huku Mkakati wa muda mfupi ni kuagiza Sukari nje ya nchi hususan katika kipindi ambacho viwanda havizalishi.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Biashara,Viwanda ,Kilimo na Mifugo Mhe. Deo Mwanyika amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuangalia changamoto zinazopelekea kushuka kwa uzalishaji wa sukari katika Viwanda mbalimbali nchini ambapo amekiri kuwa Mvua ziaoendelea kunyesha ambazo zimeongezeka kutoka mililita 200 hadi kufikia mililita 760 zimesababisha Miundombinu ya Barabara za na mashamba yenyewe kujaa maji suala lililopelekea usalishaji kusuasua.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa