Kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuli katika daraja la Kiegeya na kuagiza kujengwa kwa jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Magubike Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale amesema Halmashauri imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo hilo na kufikia ngazi ya kumwaga zege ambapo linategemewa kukamilika ifikapo mwezi wa sita mwaka huu .
Mwambambale amesema jengo hilo linatarajiwa kujengwa na kukamilika kwa takribani shilingi milioni mia moja ambazo zinategemewa kupatikana kwa kubana matumizi katika vifungu mbalimbali kwani halikuwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020, hivyo kupitia fedha hizo jengo hilo linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili na tayari kiasi cha shilingi milioni 40 kimeshatengwa kwa ajili ya kazi hiyo na kuhamishiwa katika akaunti ya kijiji cha Magubike na kwamba jengo hilo litakapomilika kinategemewa kuhudumia wananchi toka kata saba zilizo jirani na kata ya Magubike ambapo jengo hilo linajengwa.
Naye mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Sebastian Kamonga amesema anashukuru kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo kwani wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya upasuaji inawalazimu kwenda vituo vya jirani kama hospitali ya Berega ambayo iko umbali wa kilomita kumi kutoka Magubike hivyo kuwa na changamoto ya namna ya kuwasafirisha wagonjwa lakini kupitia ujenzi wa jengo huo wanatarajia kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji huduma ya upasuaji katika kituo hicho badala ya kuwasafirisha huku Injinia wa ujenzi anayesimamia ujenzi huo Samweli Baraka amesema kazi ya ujenzi inakwenda vizuri na wanapata ushirikiano wa kutosha toka kwa wananchi ambapo kwa sasa wanamalizia kazi ya kumwaga zege ili kazi ya kupandisha kuta ianze.
Sambamba na hayo wananchi wa kata ya Magubike pamoja na diwani wa kata hiyo Mh.Ernest Chilolo wamesema kutokuwepo kwa jengo hilo ni changamoto kubwa kwani wananchi wa kata hiyo na maeneo yanayopakana na kata hiyo wamekuwa wakihangaika kupata huduma za upasuaji kwa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za upasuaji na kwamba ujenzi wa jengo hilo kwao ni kama muujiza na wanashukuru kuwa kilio chao kimesikika kwani nyakati nyingine kinamama walikuwa wakihangaika kwenda kufata huduma maeneo mengine jambo lililokuwa likiwagharimu sana na kwamba katika ujenzi huo wao kama wananchi kutokana na kufurahia uwepo wa jengo la upasuaji wanachangia nguvu kazi ili kazi iweze kukamilika kwa wakati.
kuhusu suala la vifaa wanategemea kupata v

Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa