Mbunge wa jimbo la Kilosa Mh. Prof. Palamagamba Kabudi kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Kilosa amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mh. Samia Suluhu Hassan kwa fedha mbalimbali za maendeleo ambazo Wilaya ya Kilosa imekuwa ikipata ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Kabudi ametoa shukrani hizo wakati wa kikao cha baraza cha Baraza la Madiwani ambapo amesema fedha hizo zimekuwa zikifanya kazi kubwa ikiwemo shilingi milioni 160 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa daraja katika eneo la Ruhemba kwa ajili ya watembea kwa miguu, waendesha pikipiki na baiskeli jambo ambalo litasaidia wananchi kutatua tatizo la mawasiliano.
Aidha amesisitiza viongozi kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 ambapo pia amebainisha uwepo wa mkakati wa kuipandisha hadhi shule ya sekondari Mazinyungu kuwa na hadhi ya kuwa shule ya sekondari ya kutwa kwa wanafunzi wote wa Wilaya ya Kilosa na kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita mpango ambao upo kwa kwa mwaka wa fedha ujao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa