Imeelezwa kuwa ujenzi wa reli ya kisasa- SGR umeleta faida mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Kitaifa na mkakati wa nchi kuinua sekta mbalimbali za kimkakati ili nchi yetu ifikie uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kuwa na hatua muhimu kiuchumi kwa kuwa na miundombinu imara ikiwemo ya reli.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh Mhandisi Atashasta Nditie wakati wa uzinduzi wa kazi ya uchorongaji milima kwa ajili ya mahandaki yatakayotumika kupitisha reli ya kisasa ambapo amesema kuwa kazi ya uchorongaji handaki eneo la Kilosa lenye urefu wa meta 1,031 linatarajiwa kuwa handaki refu kuliko yote nchini.
Akieleza faida zitokanazo na ujenzi wa reli Mh Nditie amesema kuwa miongoni mwa faida hizo ni upatikanaji wa ajira 3,165, kukua kwa vipato vya watanzania wanaotoa huduma mbalimbali katika mradi, kukua kwa pato la taifa na sera ya viwanda ambapo umeongeza mahitaji makubwa ya vifaa vya ujenzi, pamoja na hayo sekta ya usafirishaji imefaidika kwa baadhi ya watanzania kukodisha vyombo vya usafirishaji wakiwemo wakandarasi wazawa kutoa huduma za kikandarasi za ujenzi
Sambamba na hayo kumekuwa na ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari lakini pia mradi utapunguza gharama za usafirishaji mizigo na kuifanya bandari ya Dar es salaam kuhimili ushindani pamoja na uchochewaji uanzishwaji wa viwanda maeneo mengine ya nchi kwa kutoa uhakika wa usafirishaji wa malighafi na bidhaa, pia mradi utachochea uanzishwaji wa makazi na miji midogo katika sehemu zinazojenga stesheni ambazo zitakuwa kivutio kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa shirika la reli linaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuthubutu na kuanzisha ujenzi wa reli ya kisasa kwa maendeleo ya nchina kwamba stesheni kubwa zitajengwa maeneo ya Kilosa mjini na Dodoma mjini na kwamba usanifu unaendelea ambapo umezingatia mazingira na asili ya Tanzania huku akibainisha kuwa reli hiyo itatumia nishati ya umemem na itabeba uzito wa tani 35 kwa ekseli na itakuwa na mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni za abiria na kilomita 120 kwa saa kwa terini za mizigo
Naye Mbunge wa Jimbo la Kilosa Kati Mhe Mbarak Bawaziri amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua kuwa nia ya Mheshimiwa Rais wa awamu ya tano Mh John Joseph Magufuli ni njema ya kutuletea maendeleo ili tuweze kuepukana na hali ya kuwa omba omba badala yake tuwe na mali zetu wenyewe kama watanzania tutakazojivunia.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa