Imeelezwa kuwa kuzorota kwa elimu kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo wilayani Kilosa kumesababishwa na ukosefu wa ushirikiano baina ya serikali na wazazi kwa kushindwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na kutotimiza wajibu wao ipasavyo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya Adam Idd Mgoyi katika ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu Kilosa ambapo amesema kuwa kutokana na kutowajibika kwa walimu, walimu wakuu, serikali kutotoa motisha , viongozi wa vijiji na kata pamoja na ngazi ya wilaya kumesababisha anguko la elimu.
Mgoyi amesema kuwa kutokana na kushuka kwa elimu na kutokuwepo kwa mikakati madhubuti ya utatuzi itachangia kasi ya kufeli kwa wanafunzi na kukuza kizazi cha watoto wasio na tabia njema ambao hawana msaada wa familia.
Aidha amesema kuwa wastani wa ufaulu kimkoa imejiwekea 77% ambapo Kilosa imefikia 63% ambapo Serikali kuu imeanza kupiga hatua ya utatuzi wa changamoto ambapo mwaka huu imeleta walimu 77 huku Halmashauri ya wilaya ikifanya msawazo ambao ulikuwa na mwitikio hasi kwa baadhi ya walimu kung’ang’ania shule za mjini.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na Afisa Elimu Mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mwenyekiti wa CCM, Mbunge wa jimbo la Kilosa Mh. Mbarak Bawaziri katika kuhakikisha changamoto zinapungua ametoa hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.8 kwa ajili ya ununuzi wa matofali 24,000 kwa ajili ya shule ya Msingi Msowero ambayo inakabiliwa na uhaba wa majengo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Lucas Mwambambale ametoa rai kwa wazazi na kusema suala la elimu bure lisiwafanye kubweteka kuchangia masuala ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya shule hususan majengo ambapo ameahidi kumalizia maboma yote ambayo yameinuliwa kwa nguvu za wananchi ama shule.
i
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa