Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile L. Mwambambale amewataka Wakuu wa Idara na watumishi kwa ujumla kuzingatia suala la ukusanyaji mapato kwani hicho ndicho kipaumbele chake namba moja kama kiongozi wa halmashauri na kwamba kila mtumishi anawajibika katika kuhakikisha mapato yanapatikana kama inavyostahili.
Kipaumbele hicho kimebainishwa na Mkurugenzi huyo Agosti 21, 2018 wakati wa kikao cha utambulisho wake kwa watumishi mara baada ya kuripoti Halmashauri ya Kilosa ambapo amesema ili kuwatendea haki watumishi, wananchi na halmashauri kwa ujumla lazima mapato yakusanywe kutoka katika vyanzo mbalimbali pasipo kuacha chanzo hata kimoja ili watumishi nao waweze kupata stahiki zao.
Aidha katika kikao hicho ambacho Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi aliyemtambulisha mkurugenzi huyo kwa watumishi amewataka watumishi wote kuanzia ngazi ya Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi kwa ujumla kujitathmini kwa upya kwa kuangalia changamoto zinazosababisha maendeleo ya wilaya kutokuwepo kwa kuzifanyia kazi changamoto hizo na kwamba kila mtumishi azingatie mpango kazi ili Kilosa iwe ya mabadilikoili kwenda sambamba na kaulimbiu ya Kilosa mpya inawezekana
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa