Imeelezwa kuwa miongoni mwa njia sahihi za utatuzi wa migogoro ni kwa kuhakikisha usuluhishi wa migogoro unafanyika kwa kuhakikisha usuluhishi unafanyika kwa kushirikisha kikamilifu wahusika sahihi wa migogoro kwa kuangalia chimbuko la migogoro ikiwemo kutambua maslahi ya msingi katika mgogoro husika.
Hayo yamebainishwa na Justus Mulokozi mratibu wa mafunzo kuhusu matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro katika kutatua migogoro ya ardhi Tanzania yanayofanyika wilayani Kilosa kwa siku tano ambapo amesema kuwa asilimia kubwa ya malengo kinzani ndio yanayosababisha migogoro ardhi ikiwemo matumizi kwa ajili ya kilimo/mifugo, maeneo kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori au misitu hivyo ni vema usuluhisho wa migogoro ukaangalia zaidi malengo ya migogoro.
Aidha amesema kuwa katika usuluhishi wa migogoro vyanzo vya migogoro katika jamii ni ongezeko la watu, uharibifu wa mazingira, mitizamo ya kisiasa na kiitikadi pamoja na usimamizi /mgawanyo mbaya wa rasilimali mambo ambayo yasiposimamiwa vema ni mwanya wa uwepo wa migogoro.
Pamoja na kueleza chanzo cha migogoro Mulokozi amesema ni vema viongozi wa mabaraza ya ardhi katika kata na vijiji hasa upande wa migogoro ya ardhi wanaposuluhisha migogoro wanapaswa kutafuta chimbuko la migogoro na kuhakikisha katika usuluhishaji madalali hawahusiki na badala yake migogoro hiyo ihusishe wahusika halisi.
Mulokozi amesema licha ya migogoro kuwa na faida kwa baadhi ya watu lakini pia zipo athari zinazotokana na migogoro ikiwemo vifo vinavyopelekea watu kuwa uhamishoni, majanga ya njaa ambayo kwa asilimia kubwa hutokea kutokana na jamii husika kutojikita katika uzalishaji/kilimo na badala yake muda mwingi hutumika katika migogoro, uharibifu wa mali na miundombinu ya maendeleo na kuzuia maendeleo ambapo ardhi inayogombewa inasimamishwa matumizi ya kimaendeleo hadi hapo mgogoro utakapotatuliwa na kufanyika maamuzi stahiki.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa