Imeelezwa kuwa utapiamlo bado ni changamoto kubwa kwa Mkoa wa Morogoro hasa kwa watoto chini ya ya miaka mitano na wakinamama wajawazito ambapo hali hiyo inasababishwa na jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya lishe.
Hayo yameelezwa na Afisa lishe Mkoa Bi Salome Maghembe wakati wa kikao cha kamati ya lishe Wilaya kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo amesema kuwa hali hiyo kwa kiasi kubwa inatokana na watoto kupewa chakula cha aina moja hivyo kukosa baadhi ya virutubisho muhimu ambavyo mtu anatakiwa kula ili kupata mlo kamili.
Aidha amesema sababu nyingine ni ukosefu wa matunzo kwa watoto kutokana na sababu mbalimbali pamoja na uwepo wa magonjwa yanayoathiri hamu ya kula na kusababisha mtu kukosa hamu ya kula hivyo afya kudhoofika, aidha amesema kuwa udumavu umepungua kwa Mkoa wa Morogoro ingawa bado kuna watoto wengi wenye udumavu hivyo bado kuna kazi ya kufanya ili kuhakikisha watoto hao wenye udumavu wanamalizika.
Bi Maghembe amesema kuwa udumavu utaweza kupungua ama kuisha kabisa endapo mpango wa kuwepo lishe nzuri kwa siku 1000 za kwanza utazingatiwa kwa kinamama wajawazito na watoto hususan wa chini ya miaka miwili.
Kwa upande wake Mganga Mkuu Wilaya Dokta Halima Mangiri ametoa wito kwa wadau mbalimbali kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha kuwa wilaya inafanya vizuri katika kuondoa udumavu na utapiamlo katikati ya jamii ambapo kila mmoja akitimiza wajibu wake kikamilifu hali ya udumavu na utapiamlo itatoweka.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa