Imeelezwa kuwa uwazi na mbinu shirikishi ni dhana muhimu katika jamii kwani inatoa nafasi kwa wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kutambua serikali ya awamu ya tano inafanya nini kwa ajili ya wananchi lakini pia inatoa nafasi kwa kuchangia mawazo yao na kutoa ushauri.
Hayo yameeleza na Katibu Tawala Yohana Kasitila aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya katika kikao cha kawaida cha Kamati ya Ushauri Wilaya ambapo amesema kuwa uwepo wa kikao hicho unatoa fursa kwa washiriki kutoa ushauri kwa Halmashauri kwa lengo la kuleta maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Lucas Mwambambale ametoa wito kwa wadau mbalimbali wilayani kutoa ushirikiano katika kubaini mianya ya utoroshwaji wa mapato na kwamba halmashauri ipo tayari kutoa ushirikiano ili kudhibiti mianya hiyo.
Sambamba na hayo Mwambambale ameweka wazi mapendekezo ya kufutwa kwa baadhi ya vitongoji vya Mamlaka ya Mji mdogo wa Kilosa na Mikumi ambapo upande wa Mamlaka ya Mji mdogo Kilosa kutoka vitongoji 22 vilivyopo sasa hadi vitongoji 17 huku Mamlaka ya Mji mdogo Mikumi yenye vitongoji 35 ambapo vinatakiwa vipunguzwe na kufikia vitongoji 19.
Mwambambale amebainisha sifa za eneo kuwa kitongoji ni kwamba kitongoji kinapaswa kuwa na eneo la ardhi ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya wananchi ikiwemo ardhi ya kilimo, mifugo, hifadhi,vyanzo vya maji na matumizi mengineyo, pili idadi ya kaya zisipungue 150 na tatu kitongoji kinatakiwa kuwa na idadi ya watu wasiopungua 750.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa