Imeelezwa kuwa hali ya kiwango cha udumavu kutokana na hali duni ya lishe na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano nchini ambayo ni mbaya Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan aliagiza kuwepo kwa mkataba wa usimamiaji wa shughuli za Lishe kati yake na Wakuu wa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara lengo ikiwa ni kuongeza chachu ya usimamizi ili kuondokana na hali hiyo.
Hayo yamebainisha Oktoba 29 mwaka huu na mratibu wa lishe Wilaya Zaina Kibona wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa utendaji kazi na usimamizi wa shughuli za llishe ambapo amesema kuwa hali ya udumavu kwa mkoa wa Morogoro si nzuri hivyo watendaji wa kata na vijiji ni miongoni mwa wadau ambao wanaweza kuongeza nguvu katika usimamizi wa shughuli za lishe katika maeneo yao ili kuleta mabadiliko chanya, ambapo katika kikao hicho walipata uelewa wa namna mikataba hiyo sambamba na usimamizi utakaokuwa ukifanyika katika maeneo ya kazi kwa kushirikiana na wataalam mbalimbali katika kata kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya lishe hali itakayopelekea kupunguza udumavu.
Akibainisha maeneo ya vipaumbele Kibona amesema miongoni mwa maeneo hayo ni Kutengwa fedha za kutekeleza shughuli za lishe (1000 kwa kila mtoto chini ya miaka mitano, Kuandaa mpango wa kimkakati wa Lishe wa Mkoa, Utendaji kazi wa kamati za Lishe, Usimamizi shirikishi, Kusimamia ubora na usalama wa chakula, Utoaji wa nyongeza ya matone ya Vitamin A, Utoaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu (FeFo) kwa wajawazito, Kuboresha ulishaji wa watoto wachanga na wadogo na Matibabu ya Utapiamlo
Sambamba na kupata uelewa wa mikataba hiyo watendaji hao walijaza mikataba hiyo huku wakitoa rai ya kutolewa elimu ya afya na lishe bora toka kwa wataalam lakini pia wameshauri kutengwa kwa bajeti ili kuwawezesha kushiriki vizuri katika zoezi hilo la utoaji elimu ya lishe kwa kuwezeshwa kutembelea maeneo mbalimbali katika kata zao ikiwemo kupata usafiri kufikia maeneo mbalimbali katika vijiji
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa