Vijana 22 kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Kilosa wamekabidhiwa vifaa chuma vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kwa kila mmoja bure na Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na VETA kupitia Mradi wa SUMUKUVU kwaajili ya kutengenezea vihenge vya kuhifadhia nafaka lengo likiwa ni kumsaidia Mkulima kupata nyenzo sahihi ya kuhifadhia nafaka mara baada ya mavuno,na pia kujiajiri wao wenyewe
Hayo yameelezwa na Mhandisi Jeseph Kivako ambaye ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini ya mafunzo, na pia Mratibu wa Sumukuvu VETA katika kikao cha kukabidhi vifaa hivyo Agosti 11 ,2023 ambapo amesema kuwa VETA imeingia makubaliano na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kushirikiana kufundisha vijana kuondoa athari za Sumukuvu kwenye mazao ya nafaka hususan Mahindi na Karanga.
Mhandisi Kivako amesema kuwa Sumukuvu inapatikana kabla na baada ya kuvuna huku kukiwa vipengele viwili vikubwa ambavyo ni uhifadhi na ukaushaji wa mazao ambapo amefafanua kuwa Mradi huo umejikita katika uhifadhi wa nafaka hivyo Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa Tanpack pamoja na kujenga Maghala makubwa pia wameona umuhimu wa wakulima wa kawaida kupata nyenzo sahihi ya kuhifadhia nafaka ambayo ni vihenge vya chuma.
Kivako amesema kwa kuzingatia hilo VETA imetoa mafunzo kwa vijana 420 kutoka Tanzania bara na visiwani na kuwatunukiwa Vyeti ambapo kati yao vijana 22 wametoka Wilayani Kilosa na kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kutambulika,pia yatawawezesha kuwasaidia wakulima kwa kuwaelimisha juu ya faida ya uhifadhi nafaka kapitia Vehenge vya chuma,na ni matumaini yao kuwa kundi hilo litaenda kutengeneza fursa za ajira katika maeneo yao kupitia vifaa hivyo walivyopewa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba amesema kuwa Teknolojia hiyo ya uhifadhi wa nafaka kwa kutumia Vihenge hivyo itatoa suluhu ya tatizo la Sumukuvu katika mazao,hivyo amewataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii na pia kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na pia waweze kutoa ujuzi huo kwa vijana wengine katika maeneo yao
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa