Wito umetolewa kwa vijana walio chini ya mradi wa OYE kuwa chachu katika jamii kwa kuonyesha namna walivyobadilika kupitia fursa waliyoipata na kuwa viongozi wakuleta chachu ya kuhamasisha jamii kuachana na tabia potofu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa Morogoro Flora Yongolo ambapo amesema Serikali inashirikiana na taasisi mbalimbali kuboresha maisha ya watu ambapo amewasisitiza kufanya juhudii kwani wana nafasi na mafanikio huku akiwataka kupanga kufika mbali kwani inawezekana endapo watafanya juhudi.
Akizungumzia suala la mitaji Yongolo ameishauri Halmashauri kupitia mikopo inayotolewa kwa vijana kuangalia vikunmdi ambavyo vina sifa kuvipa kipaumbele na kuhakikisha vinafanya yaliyokusudiwa huku akiwataka vijana hao watakapowezeshwa kuendeleza mitaji waliyonayo jambo litakalowasaidia kuendelea kuaminiwa ambapo pia ameahidi kuzibeba changamoto walizobainisha kwa ajili ya utekelezaji.
Akieleza namna mradi wa OYE unafanya kazi Meneja Mradi Herman Hishamu amesema mradi huo unafanya kazi katika kata zaidi ya kumi katika ya Wilaya ya Kilosa na unalenga kuimarisha uchumi wa vijana na mazingira wezeshi ya kibiashara ambapo wamefundishwa stadi za maisha na kuunganishwa na taasisi mbalimbali lengo likiwa kuwakwamua na kuwawezesha kujiajiri wenyewe ambapo wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo cha mboga mboga na alizeti, ufugaji kuku, nishati, utengenezaji majiko banifu na shughuli nyinginezo ambapo kupitia hizo vijana wamekuwa wakipatia fedha za kujikwamua na kukidhi mahitaji yao.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Afisa Maendeleo ya Jamii Simforosa Mollel ameushkuru uongozi wa SNV na MJUMITA kwa namna wamekuwa msaada kwa vijana kuwawezesha katika stadi za maisha huku akiwataka vijana hao kuendelea kutumia fursa zinazojitokeza kwa kuzifanyia kazi ambapo amewasisitiza kuwatumia maafisa mbalimbali walioko katika maeneo yao ili kufikia malengo yao hususani maafisa maendeleo ya jamii, kilimo na mifugo lakini pia amebainisha kuwa fursa ya kupata mikopo ipo kwani tayari wanajua nini wanahitaji kufanya kutokana na stadi walizopata.
Wakisoma risala yao vijana walio chini ya mradi wa OYE wamesema mradi ulitoa mafunzo ya nadharia katika nyanja ya stadi za maisha,ujasiriamali,mpango wa fedha, uundaji katiba na vikundi mambo ambayo yamekuwa msaada kwao na kuwabadilisha toka kuwa bora vijana na kuwa vijana bora kwa kuwawezesha kubadilika kimtazamo na kujikwamua kiuchumi kwani kwa sasa wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufuga kuku, kilimo cha bustani na matunda, kupanda miti, kutengeneza majiko banifu, kusambaza sola za sanking na kuweka hisa ambapo wanajipatia fedha za kujikimu lakini pia wamekuwa msaada kwa vijana wengine walio nje ya mradi wa OYE. Ambapo wamebainisha changamoto zinazowakabili ni ukosefu wa mashine na mipira ya umwagiliaji, mashine ya kutotoleshea mayai na wataalam wa mifugo, masoko na mitaji.
Diwani wa Kata ya ya Ulaya Mh. Kibati
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa