• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Vikundi vilivyopata mikopo vyatakiwa kufanya marejesho kwa wakati

Posted on: June 2nd, 2023

Jumla ya vikundi 25 kutoka makundi maalum ya wanawake, vijana na  watu wenye ulemavu vilivyopata mkopo wa asilimia 10% toka katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani  vimetakiwa kutambua thamani ya mkopo huo kwa kuhakikisha vinafanya marejesho ya fedha hizo kama inavyostahiki.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Alto Mbikiye wakati wa mafunzo kwa vikundi hivyo ambapo Halmashauri imetoa mkopo wa kiasi cha shilingi 333,192,320.00 ambapo vikundi 5 vya vijana vimepata mkopo wa shilingi 58,838,400.00, vikundi 12 vya wanawake shilingi 234,596,640.00 na vikundi 8 vya watu wenye ulemavu wakipata mkopo wa shilingi 39,757,280.00 ambazo zinapaswa kuwasaidia katika kuinua kipato chao.

Mbikiye amevitaka vikundi hivyo kufanya marejesho ya fedha hizo kwa wakati kwani mkopo huo hauna riba na kwamba kila kikundi kinapaswa kufanya marejesho kupitia namba ya malipo(control number) ambazo kila kikundi kimepewa namba ambazo ndizo zitatumika kipindi chote cha muda wa mkopo.

Pamoja na msisitizo huo vikundi hivyio vilipata mafunzo katika nyanja mbalimbali kupitia wataalam toka benki za NMB na CRDB pamoja na wataalam toka idara za biashara, kilimo na mifugo, sheria, ustawi wa jamii, TAKUKURU na Maendeleo ya Jamii, lengo ikiwa ni kuwawezesha kuendana sawasawa na maombi na makusudi ya mkopo ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Aidha wawakilishi mbalimbali toka makundi ya vijana, wanawake na wenye ulemavu waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja wametoa shukrani zao kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Uongozi wa Halmashauri chini ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwatazama kwa jicho la tatu na kuwawezesha kwa fedha ambazo wameahidi kuzitumia kwa malengo yaliyokususdiwa na kuzirejesha kwa wakati kwani Serikali imewaamini na kwamba wanaamini zitawasaidia kuwainua katika vipato vyao na kuwaletea maendeleo.


Tangazo

  • TANGAZO LA KONGAMANO LA VIJANA WILAYANI KILOSA April 04, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 07, 2025
  • RC MALIMA AWATAKA WAAJIRI MOROGORO KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WAO

    May 01, 2025
  • WALIMU WAPYA 74 WILAYANI KILOSA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU MAADILI NA HAKI ZA UTUMISHI WA UMMA

    April 29, 2025
  • KILOSA YABORESHA USIMAMIZI NA UFATILIAJI WA MIKOPO YA 10% KWA UNUNUZI WA GARI JIPYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa