Wakati janga la ugonjwa wa corona likiendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ameitaka jamii kufahamu kuwa ugonjwa wa corona ni ugonjwa hatari hivyo amewataka viongozi wa dini, tarafa, kata na vijiji kuendelea kuzingatia taratibu za kudhibiti zinazoelekezwa na wataalam wa afya kwa kuhakikisha taratibu hizo zinasimamiwa ipasavyo katika maeneo wanayoyasimamia lengo ikiwa ni kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Mgoyi amesema hayo wakati wa kikao chake na viongozi mbalimbli wa dini, maafisa tarafa na watendaji wa kata ambapo ametaka kila mmoja kuwajibika kwa sehemu yake kwa kuhakikisha taratibu zote zilizoelekezwa zinafanyika na kufuatwa ambapo amesema sheria za mbalimbali ikiwemo za afya, sheria ndogo, sheria za usafi na nyinginezo zinafuatwa hususani taratibu za kufuata ili kudhibiti maambuklizi ya virusi vya corona kama zinazovyoelekezwa na wataalam wa afya pamoja na kuzingatia unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni, katika kudhibiti virusi vya corona zinazopaswa kufutwa, ukaaji wa umbali wa mita moja toka mtu mmoja kwenda mtu mwingine na sheria nyinginezo.
Pamoja na hayo Mgoyi amesema ipo haja ya kuendelea kukumbushana na kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa sehemu yake ndani ya jamii anayoingoza na kwamba wilaya ya Kilosa ina njia nyingi za watu kuingia katika wilaya hivyo ni vema umakini ukaongezeka katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwani ugonjwa huu ni hatari na kwamba shughuli zote katika jamii hazizuiwi isipokuwa kila mmoja anapaswa kuzingatia sheria na taratibu huku akiwataka viongozi hao kuzingatia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa jamii wanayoingoza huku akisema kuwa kwa yoyote ambaye hatazingatia sheria hizo eneo lake litafungiwa.
Aidha amewataka watendaji wa kata na maafisa tarafa kuhakikisha wanafanya wajibu wao ipasavyo na kwamba mtendaji yoyote ambaye hatawajibika katika nafasi yake hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake huku akitoa wito kwa wadau na wafanya biashara mbalimbali kuungana na wilaya kwa ujumla katika kuchangia mahitaji mbalimbali ya vifaa kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona ambapo pia amewataka wamiliki wa vituo vya afya na zahanati binafsi kuunga mkono juhudi za wilaya katika kudhibit virusi vya corona kwa kutoa michango yao ambapo pia amesema kwa vyombo vyote vinavyosafirisha abiria ikiwemo noah na mabasi kutakuwa na utaratibu wa upuliziaji dawa katika vyombo hivyo kila vyombo hivyo vinapoingia wilayani.
Naye Katibu Tawala Wilaya Kilosa Yohana Kasitila amesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuingoza jamii kwa kumuomba Mwenyezi Mungu ili atunusuru katika janga la corona na kwamba viongozi hao wanao wajibu wa kushirikiana na wilaya katika kuwasaidia wananchi walio chini yao kwa kuhakikisha wanashiriki katika nyumba za ibada kwa kukaa katika umbali unaotakiwa, kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni ili waweze kumwabudu Mungu wakiwa salama ambapo upande wa watendaji wa kata na maafisa tarafa wametakiwa kusimamia maeneo yao kwa kuendelea kuhamasisha jamii kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa