Agosti 28 mwaka huu Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila ametoa wito kwa viongozi wa vitongoji, vijiji na kata kuzisimamia vyema sheria ndogo za hifadhi ya mazingira za Halmashauri kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kutokana na kutosimamia vema kwa sheria hizo.
Kasitila ametoa wito huo katika kikao cha viongozi wa tarafa za Masanze, Ulaya na Kimamba ili kujadili utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo amewataka viongozi hao kuhakikisha wanazisimamia sheria hizo na kutoa elimu kwa wananchi juu ya sheria ndogo za Halmashauri ili kuepusha migogoro.
Naye mwanasheria Daniel Mwamlima amesisitiza utolewaji elimu juu ya sheria hizo kwa wananchi kwani kwani wao ndio watumiaji wakubwa wa sheria hizo kwani endapo wananchi watazitambua sheria na kuzifanyia kazi wataepukana na migogoro ikiwemo kuhakikisha mifugo kutozurura hovyo na kufanya uharibufu ambao utapelekea uwepo wa faini sambamba na uhifadhi wa mazingira na kutunza vyanzo vya maji.
Afisa wa TAKUKURU Bw Msigwa amesisitiza viongozi hao kusimama katika nafasi zao na kuepuka vitendo vya rushwa sambamba na kusimamia kuundwa/kuhuishwa kwa kamati za amani pamoja na za ulinzi na salama ambazo zinawajibu wa kushughulikia migogoro inayojitokeza vijijini.
Kamanda wa polisi Mapalala amesisitiza kamati za ulinzi na usalama vijijini kufanya kazi inavyostahili lakini pia amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano katika utendaji kazi.
Afisa utumishi Noel Abel amewataka viongozi hao kuzingatia utawala bora na kutatua changamoto kwa kufuata ngazi husika lakini pia kuimarishwa kwa kamati za ulinzi na usalama.
Baada ya majadiliano katika kikao hicho Mkuu wa idara ya mifugo dkt. Yuda amesisitiza kila kijiji kuwa na mwongozo wa namna ya kukabiliana na migogoro, kila mtendaji wa kata/kijiji awe na sheria ndogo za halmashauri, uwepo wa doria za mara kwa mara, kuwepo kwa ubainishwaji wa njia za kupitisha mifugo ambazo hazipasi kufungwa ama kulimwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa