Serikali Wilaya ya Kilosa mkoa Morogoro kwa kushirikiana na Viongozi wa Dini na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza upya zoezi la kutoa elimu kuhusu faida za Chanjo ya UVICO 19 baada ya takwimu za hali uchanjaji kutoridhisha.
Akieleza hali ya uchanjaji hadi sasa Mganga Mkuu Wilaya ya Kilosa Dokta George Kasibanee amesema Wilaya hiyo ina zaidi ya wakazi laki tano (500,000) huku matarajio kuchanja watu laki tatu na elfu ishirini (320,000 ) ambapo hadi sasa waliochanja ni watu elfu ishirini na nne tu (24,911) jambo ambalo haliridhishi.
Dkt. Kasibante amesema mpango wa Serikali ni kufikia asilimia sitini kwa watu waliochanja hivyo wameona ni vyema kushirikisha viongozi wa dini ,na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaushawishi mkubwa katikati ya jamii.
Kwa niaba ya viongozi wa dini Shekhe Milambo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu na chanjo ili kuwa na afya njema huku akitolea mifano baadhi ya nchi ikiwemo Saudi Arabia ambayo hairuhusu waumini wa dini ya kiislam kuingia katika nchi hiyo ili kutekeleza ibada ya hijja kutokana na hofu ya ugonjwa wa corona ambao umesababisha vifo vingi, sambamba na hayo amesisitiza wanachi kushiriki zoezi la sensa pindi litakapoanza ifikapo mwezi wa nane mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa