Novemba 11 mwaka huu imeelezwa kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya Kilosa imekuwa ikikumbwa na migogoro ya ardhi baina ya mipaka kijiji na kijiji, wakulima na wafugaji na migogoro ya mtu na mtu ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kutokana na muda mwingi kuchukuliwa na utatuzi wa migogoro badala ya kufanya shughuli za maendeleo, hivyo amewataka washiriki wa mafunzo ya matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro kuyafanyia kazi yale watakayojifunza katika mafunzo hayo jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa migogoro ama kupunguza migogoro.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro katika kutatua migogoro ya ardhi ambapo amesema kuwa nyakati nyingine migogoro hiyo imekuwa ikishindwa kutatuliwa kutokana na upendeleo ambao umekuwa ukifanyika kutokana na kukosa uadilifu ikihusisha masuala ya rushwa au kutokujua njia sahihi za utatuzi wa migogoro hiyo.
Mgoyi amesema kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea kushindwa kutatuliwa kwa migogoro hiyo ni ushiriki hafifu wa viongozi wa halmashauri kwa kuwaachia serikali za vijiji na watendaji wa kata kushughulikia migogoro, hivyo ametoa rai kwa washiriki hao kuyafanyia kazi yale watakayojifunza kwa kuhakikisha wanaanza na kutafuta suluhu na
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa