Viongozi wa Vyama vya Siasa Wametakiwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mwaka huu ili waweze kuhakiki na kurekebisha taarifa zao.
Hayo yameelezwa na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la kilosa na mikumi Ndg. Betuely Ruhega wakati wa kikao cha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili kilichofanyika Bomani Mei 6, 2025 ambapo amewasihi kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo muhimu ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba mwaka huu.
Betuely ameongeza kuwa sambasamba na zoezi hilo wawasilishe orodha ya mawakala wa uandikishaji wapiga kura kabla au ifikapo Mei 12, 2025 watakaosimamia na kufatilia kanuni, sheria na taratibu za uchaguzi zinazingatiwa katika vituo husika.
Kwa Upande wake Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kilosa Bi. Simforoza Mollel amesema jimbo la kilosa na Mikumi litakuwa na vituo vya uandikishaji 53 na pia zoezi hilo litafanyika kwa kila kata na vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10: 00 ni jukumu la viongozi hao kuendelea kuelimisha wananchi umuhimu wa kuhakiki na kurekebisha taarifa zao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa