Katika hali ya kukabiliana na lishe duni kwa watoto wachanga na wanafunzi, Wahe. Madiwani na viongozi wote kuanzia ngazi ya kata, vijiji na vitongoji wametakiwa kuhimiza ulaji sahihi kwa watoto ikiwemo shuleni ili kuongea kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi pamoja na kupunguza udumavu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mhe. Wilfred Sumari Mhe. Sumari ameyasema hayo hivi karibuni katika Mkutano wa baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa FDC Ilonga ambapo amewataka viongozi hao kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao.
Kwa Upande mwingine katika baraza la mwaka la Madiwani limefanya uchaguzi wa kumpata makamo mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambapo makamo kwenye kiti aliyemaliza muda wake Mhe. Hassan Mkopi amefanikiwa kuchaguliwa tena kwa zaidi ya 90% ya kura zote zilizopigwa na hivyo kuendelea kushika nafasi hiyo ambapo baada ya kutangazwa mshindi Mhe. Hassan Mkopi amewashukuru Madiwani kwa kumchagua na kumuamini tena kuwa makamo mwenyekiti.
Vilevile Baraza hilo la Mwaka limeweza kufanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za halmashauri ya wilaya ya Kilosa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa