Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka H. Shaka amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya Kilosa kutimiza wajibu na kutenda haki ili kulinda maslahi ya Wananchi na kusisitiza kuwa Serilkali haitamvulia kiongozi yeyoteambaye atashindwa kusimamia upatikanaji wa haki.
Mhe. Shaka ameyasema hayo 26 Oktoba, 2023 wakati akiongea na Wananchi wa kata ya Kimamba B katika mkutano wa hadhara uliolenga kujadili shughuli za maendeleo na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa eneo hilo ambapo amebainisha kwa kusema kuwa changamoto za migogoro ya ardhi na ya Wakulima na wafugaji kwa asilimia kubwa zimetokana na baadhi ya viongozi wa vitongoji na vijiji kutotimiza wajibu wao.
Aidha amesema kuwa migogoro inaongezeka Wilayani hapa kutokana na viongozi kukiuka maadili na kutotenda haki hivyo ameonya kuwa kila kiongozi aliyepewa dhamana anawajibika kuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi kwa kusimamia haki.
Amewataka baadhi ya Viongozi wenye tabia ya kupokea rushwa ili kutoa upendeleo flani kuacha mara moja kwani ni ukiukwaji wa Sheria na pia ni chanzo cha migogoro ambayo inaonekana kukithirikatika maeneo mbalimbali Wilayani hapa na kusisitiza kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa atakayebainika kufanya hivyo.
Sambamba na hayo amewaonya baadhi ya wafugaji wenye tabia ya kulishia mifugo kwenye mashamba ya Wakulima na kutembeza mifugo hovyo katika maeneo ya mijini kuacha mara moja kwani hiyo inachochea vurugu,migogoro na uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Costantine Nzila amewasisitiza wananchi kufuata sharia na taratibu zilizowekwa ili kuepuka migogoro ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma shughuli za maendeleo na pia kuleta uvunjifu wa amani.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa