Waandikishaji wasaidizi wametakiwa kufanya kazi kwa uaminifu kwani wao ni sehemu ya tume katika kipindi cha uandikishaji hivyo wafanye kazi ya uandikishaji kwa uaminifu na uadilifu ambapo wanapaswa kuhakikisha zoezi linafanyika kwa usahihi na kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi iko pamoja nao na kushirikiana nao kwa ukaribu.
(JAJI MTSAAFU) KAMISHNA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI MARY H.C.S LONGWAY AKITOA RAI KWA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI
Rai hiyo imetolewa Februari 01 mwaka huu wakati wa mafunzo kwa waandikishaji na Jaji Mstaafu Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mary H.C.S. Longway kwa waaandikishaji wasaidizi na BVR Operators katika kutekeleza kazi ya uandikishaji amewataka kuwa waadilifu, wasikivu na uaminifu wa hali ya juu ambapo amesema uadilifu, usikivu na umakini katika kazi ya uandikishaji utasaidia kutoharibu daftari la kudumu la wapiga kura hivyo ni vema wakatambua kuwa wanafanya kazi kwa niaba ya Tume na kwamba Tume inawaamini na inawategemea.
Pia amewataka kutambua kazi ya uandikishaji ni kazi ya kipekee kwani wanawafikia watu wengi kwa kuhakikisha kila anayestahili kuandikishwa anafanya hivyo lakini pia kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kwa kuwajulisha watu wanaoishi nao juu ya zoezi linaloendelea ili wapate haki ya kikatiba ya kujiandikisha na kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu ambapo pia amewataka kuanza kazi kwa wakati kwa kuanza kazi saa mbili kamili asubuhi na kufunga zoezi saa kumi na mbili jioni.
Usikivu na uadilifu na umakini katika uandikishaji ni muhimu hivyo ni vema ikazingatiwa katika uandikishaji wa majina na taarifa za watu kwa usahihi lakini pia kuwa makini katika na kuhakikisha mashine zinakuwa katika hali nzuri ikiwemo kuhakikisha picha za wateja zinaonekana vizuri kwani sura na ndiyo inayohitajika zaid kwa ajili ya utambulisho. Kamishna amesisitiza.
Pamoja na hayo amewataka kuwa makini katika utunzaji wa vifaa vya uandikishaji ikiwemo mashine ya BVR , fomu zote za uandikishaji kwani gharama zake ni kubwa hivyo vinapaswa kutunzwa na kuwa na uangalifu mzuri katika matumizi na kuvitunza lakini pia amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano pindi wawapo katika vituo vyao vya kazi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa