Katika kuhakikisha Waathirika wa mafuriko wilayani Kilosa wanapata huduma muhimu Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kwa Kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wamekabidhi misaada mbalimbali kama vile chakula, mavazi, malazi na vyombo ili waweze kujikimu katika kipindi hiki kigumu.
Misaada hiyo imetolewa Disemba 20 na 21,2023 katika kata za Tindiga, Malangali, Rudewa na Mvumi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilosa Bi. Salome Mkinga ambapo amesema misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali walioguswa kwa lengo la kuwafariji waathirika hao ambao wamekumbwa na adha ya mafuriko na kusababisha uharibifu wa mali zao.
Baadhi ya Wananchi waliopatiwa Misaada hiyo wametoa shukrani zao za dhati kwa wadau mbalimbali walioguswa na kutoa misaada hiyo na kusema kuwa itawasaidia katika kipindi hiki kigumu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa