Wito umetolewa kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwajibika ipasavyo kila mmoja katika eneo lake kwa kutumia mbinu shirikishi ya utendaji kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi na wilaya kiujumla.
Wito huo umetolewa Septemba 28 mwaka huu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ameir Mbarak katika mkutano wa Kamati Kuu ya CCM lengo ikiwa ni kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo ya miradi iliyotembelewa na Kamati ya Siasa Wilaya hivi karibuni .
Ameir amesema kuwa watendaji wa kata kwa kushirikiana na waheshimiwa madiwani wahakikishe kila wanapoandaa taarifa zao kabla ya kuziwasilisha katika baraza la madiwani na maeneo mengine wanao wajibu wa kuhakikisha taarifa hizo zinakuwa sahihi na kujiridhisha kwa kusimamia kwa kina na kuwapa wananchi haki ya kusomewa taarifa za mapato na matumizi katika kata na vijiji vyao.
‘‘Aidha niseme kuanzia sasa kamati ya siasa itakuwa inawajibika kusimamia miradi inayoendelea na itakayokuwa ikiendelea katika kata zote ili kuongeza nguvu ya kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuwaachia baadhi ya watalamu na madiwani na niendelee kusisitiza wataalam ongezeni nguvu ya kuwashirikisha waheshimiwa madiwani katika miradi hasa ya TASAF ambayo imebainika kuwa na ushirikishwaji mdogo wa madiwani’’.Ameir ameongeza
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa