Afisa Tawala Wilayani Kilosa Bi Anjalla Mono amewataka wakina mama kuhakikisha wananyonyesha watoto wao ipasavyo ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali kwani maziwa ya mama yana virutubisho sahihi kwa Mtoto.
Rai hiyo imetolewa Agosti 11,2023 wakati wa kilele cha siku ya unyonyeshaji yaliyofanyika katika viwanja vya kliniki ambapo amesema kuwa virutubisho vinavyopatikana katika maziwa ya mama vinasaidia katika ukuaji wa mtoto kiakili na pia humjenga mtoto inavyostahiki.
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya Bi Zaina Kibona amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuongeza uelewa na kuelimisha juu ya umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama kwa mtoto kwa kipindi stahiki.
Pia amewataka kina mama kunyonyesha kina kwa kufuata taratibu za unyonyeshaji kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya ya Mama na Mtoto na kuhakikisha mama anapata mlo kamili ili aweze kuzalisha maziwa kwa Wingi.
Kwa upande wake Mratibu wa chanjo Wilaya Bi Rakhia Ngayungwa amewataka kinamama hao kuzingatia utaratibu na upatikanaji wa chanjo kwa Watoto na kuhakikisha wanapata chanjo zote kama taratibu zinavyoelekeza ili kuwawezesha watoto kukua vizuri
kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Saidia unyonyeshaji,Wezesha wazazi kulea Watoto na kufanya kazi zao kila siku’’
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa