Kufuatia kufutwa kwa mashamba na kurejeshwa kwa wananchi Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuhakikisha inapima mashamba hayo na kuwa na hati kubwa itakayosoma Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Wizara ya Kilimo na kisha kugawiwa kwa wananchi.
Mh. Bashe ameyasema hayo Februari 4, 2023 katika ziara yake ya siku moja wilayani Kilosa katika kata ya Mvumi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu CCM la kumtaka Waziri huyo kufika Kilosa ili kutatua changamoto za wananchi juu ya mashamba yaliyofutwa na Serikali na kukabidhiwa kwa Halmashauri ili iyagawe kwa wananchi ambapo amesema kuwa maelekezo ya Serikali ni kuwa na hati kubwa ambapo ili yanapokabidhiwa kwa wananchi lazima yawe na hati ndogo itakayokabidhiwa kwa kila mwananchi atakayepimiwa eneo kwenye mashamba hayo ambapo uwepo wa hati hizo utadhibiti mashamba hayo kutouzwa.
Sambamba na hayo Bashe amesema kugawiwa kwa mashamba hayo kwa wananchi wa maeneo husika badala ya kukodishwa kutasaidia wakulima kutovamia mashamba ya watu wengine lakini pia wananchi wanapokuwa na mashamba yao itawasaidia kutokuwa manamba kwenye mashamba ya wengine.
Nao wananchi wa kata ya Mvumi wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi huo uliotolewa kwani mashamba hayo yatawasaidia kupata kipato na kupunguza umaskini.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa