Baadhi ya Vikundi vya wakulima kutoka kata ya Malolo na Maguha Wilayani Kilosa wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutunza Bayoanuai za Kilimo na kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya ufugaji nyuki ili waweze kufanya shughuli zao za tija.
Makabidhiano hayo yamefanyika Januaruari 24,2024 Katika kata ya Maguha ambapo vifaa vilivyogawiwa ni pamoja na Mizinga ya nyuki, Tanki za kuifadhia asali, Bomba la moshi, Mavazi maalum ya kuvaa wakati wa uvunaji, wavu wa kuchujia asali, Patasi na kifagio ikiwa ni ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EUROPEAN UNION) chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (FAO)
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo katika ukumbi wa Kata ya Maguha Afisa Tarafa ya Magole bi Asha Saidi Amani ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka amevipongeza vikundi hivyo kutoka kata ya maguha na Malolo kwa hatua hiyo kubwa na kwamba Mradi huo utaleta manufaa kwa wananchi wa kilosa na hata nje ya kilosa .
Pia amewataka wakulima hao wawe mabalozi kwa wengine na mfano wa kuigwa kwa kuendeleza mafunzo waliyopata pamoja na kusimamia vifaa walivyokabidhiwa kwa kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kuwaelimisha na kupitia mafunzo waliyopatiwa kutoka kwa wawezeshaji wa mradi huo na kuleta mafanikio hasa katika utunzaji wa mazingira katika maeneo yao na maeneo mengine ndani ya kilosa.
Sambamba na hayo Bi. Asha amependekeza Ofisi ya Mkurugenzi iwapatie wakulima hao eneo maalum la kuuza bidhaa zao za asali hiyo itawasaidia wakulima hao kujiendeleza kiuchumi na kujisimamia wenyewe.
Bi. Asha ameongeza kwa kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza mradi huo wa utunzaji wa mazingira kwa kuingia mikataba na mashirika husika mpaka kufikia katika maeneo yao na kuwa moja kati ya wanufaika
wa mradi huo.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi Diomedes Kalisa kutoka shirika la kilimo na chakula la umoja wa mataifa (FAO) amesema kuwa kupitia mradi huo wa kuwajengea uwezo wakulima kutunza bayoanuai za kilimo hasa katika utunzaji wa mazingira amewataka wakulima hao watumie fursa hiyo vizuri kupitia
Naye Afisa nyuki wa wilaya Bi. Diana Sunday Mahimbali amesema kuwa mradi huo utaleta tija kwa wakulima hao kupitia Mafunzo na vifaa hivyo walivyokabidhiwa ambapo italeta uzalishaji bora wa mazao ya nyuki ukilinganisha na kipindi cha nyuma, pia itawawezesha kujiendeleza kiuchumi kupitia zao la asali katika ufugaji wa huo wa nyuki.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa