Rai imetolewa kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali mbalimbali kujikita zaidi katika kuwatambua kwa kina wadau na wateja wa bidhaa mbalimbali wazozalisha kwani itawasaidia kutambua ukubwa wa soko walilonalo.
Rai hiyo imetolewa Agosti 2, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Abel. Busalama wakati wa Maonesho ya Nane Nane alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na kujionea bidhaa zilizopo katika banda hilo ambapo amesema ipo haja ya kufahamu ukubwa wa soko jambo ili kujua kiwango cha uzalishaji kitakachoendana na mahitaji pamoja na tija kwa jamii.
Aidha ameshauri wataalam wa kilimo, mifugo na uvuvi kuongeza ukaribu kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali kwa lengo la kuendelea kutoa ushauri wa kitaalam namna ya uzalishaji sambamba na upatikanaji wa masoko ndani na nje ya wilaya.
Licha ya ushauri huo lakini pia amepongeza wadau na wajasiriamali walio na bidhaa katika banda la halmashauri kwa namna walivyoonyesha juhudi katika uzalishaji na kushiriki maonesho hayo ili kupata fursa za kutangaza bidhaa na kujifunza jambo litakalosaidia kupata masoko katika maeneo mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa