Mradi wa uwajibikaji jamii katika ufatiliaji wa rasilimali za umma ulio chini ya mtandao wa wakulima wadogo Tanzania unaofadhiliwa na SDC katika uboreshwaji na utolewaji wa huduma za ugani kupitia maafisa ugani ambao watakuwa wakitoa elimu kwa wakulima kwa mbinu za kiikolojia kwa kuhakikisha huduma za ugani ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kilimo hivyo kuwasaidia wakulima hususani wanawake kwa kuboresha huduma za ugani.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa MVIWATA kanda ya kati Morogoro Joseph Sengasenga ambapo amesema mradi huo wa miaka minne utafanya kazi katika vijiji vitano vya Mhenda, Ilonga, Ulaya, Madudu na Rudewa Gongoni ambapo amesema mradi huo unalenga suala zima la uwajibikaji baina ya wapokea huduma ambao ni wakulima na watoa huduma ambayo ni Serikali ambapo huduma zitakazotolewa zinalenga katika kuboresha maisha ya jamii nzima ambapo jamii na Serikali kila moja kwa eneo lake akiwajibika italeta matokeo chanya katika sekta ya kilimo na kuleta tija kwa Serikali kwa kukusanya mapato huku jamii ikifaidika na utatuzi wa changamoto zinazowazunguka.
Akizungumzia maazimiao yaliyofikiwa baada ya matumizi ya pima kadi iliyofanyika katika vijiji hivyo ili kubaini changamoto na mapendekezo yaliyojitokeza Sengasenga amesema imebainika kutokuwepo kwa mashamba darasa katika baadhi ya vijiji ambayo yanapaswa kuanzishwa ili kueneza ujuzi na maarifa ya kilimo cha mazao tofauti tofauti kwa wakulima jambo litakalosaidia wakulima kulima kwa tija.
Naye kaimu mkuu wa wilaya Reginald Simba ametoa rai kwa wakulima kutambua kuwa serikali haifanyi kazi peke yake bali inafanya kwa kushirikiana na wadau m,mbalimbali hivyo amewataka wakulima mbalimbali wilayani kilosa kutumia kwa tija fursa ya uwepo wa wadau mbalimbali na kuendeleza jitihada za serikali sambamba na za wadau mbalimbali kwa kuendeleza mema yoteb yanayotolewa na wadau hao ili kuendelea kupata tija.
Simba amesema ni vema wanakilosa wakawa mstari wa mbele katika kufikia malengo kwa kuhakikisha wanaepukana na kilimo cha mazoea ambapo kimekuwa kikifanyika kwa muda mrefu na kusababisha kudumaa kimaendeleo kwani hulka ya kutobadilika ni kikwazo cha kutosonga mbele hivyo ni vema kuwatumia watalaam na kwamba maendeleo yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja kwa kushirikiana na Serikali.
Pamoja na hayo Simba amesema anategemea kuwa kupitia mradi wa MVIWATA wakulima hao watapiga hatua na kubadili fikra zao kwa kuziangalia changamoto zinazowakabili kama fursa na kuzitafutia ufumbuzi ambao uko ndani ya maeneo yao hivyo ili kuzikabili changamoto hizo ni vema wakajipanga namna ya kuzikabili na kuzipatia majibu stahiki ikiwemo suala la ujazo wa lumbesa ambao wakulima wakiweka nia na msimamo wa pamoja kutouza mazao kwa lumbesa jambo ambalo linawezekana.
Naye Afisa Utumishi na Utawala Noel Abel akizungumzia upande wa changamoto ya kutofanyika kwa vikao vya kisheria amesema viongozi wa vijiji wanakumbushwa kuhakikisha vikao vya kisheria vinafanyika inavyostahiki na kwamba kamati ya huduma za jamii inao wajibu wa kuweka ajenda za changamoto za wakulima kama vile ugawaji ardhi na kutenga maeneo lakini pia ipo haja ya halmashauri ya kijiji kusimamia matumizi ya ardhi, ufugaji na masuala mbalimbali ya wakulima hivyo halmashauri ya kijiji isimamie uanzishwaji wa shamba darasa kwa ajili ya wakulima.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa