Wakulima Wilayani kilosa hususan Vijina na Wanawake wanatarajia kunufaika na Mradi utakaowawezesha kuongeza tija ya uzalishaji na upatikanaji wa masoko (FEIPA) unaoendeshwa kwa ushirikiano wa shirika la Kilimo tija na Kampuni ya Green Intergration wenye lengo la kuwawezesha wakulima katika masuala ya Teknolojia,Masoko,pamoja na ujasilia mali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa Juni 6 mwaka huu na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Green Intergration Bwana Ayub Eliah wakati akitambulisha Mradi huo kwa Wadau mbalimbali wa Kilimo ambapo amesema Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa Wilayani hapa kwa kipindi cha miaka 3 na kunufaisha Wakulima takribani 800 kutoka maeneo mbalimbali.
Amesema kuwa Mradi huo umejikita kwenye maeneo manne ikiwemo utoaji wa Elimu ya huduma za ugani kwa Wakulima, kuwawezesha wakulima kupata Teknolojia bora za uzalishaji wa Mazao, kuwawezesha Wakulima kupata Rasilimali fedha kwaajili ya Uendeshaji wa Shughuli za Kilimo, pia kuwaunganisha Wakulima na masoko hivyo amewataka Wakulima kuchangamkia Fursa hiyo ili kufanya Kilimo chenye tija.
Hata hivyo amesema kuwa Mradi huo utaendeshwa kwa kuchangia Gharama ambapo Kampuni itachangi asilimia 60 na mradi utachangia asilimia 40,ambapo amebainisha kuwa Watafanya kazi na vikundi vilivyopo na vipya kwa kuzingatia uhalali na uhai wa vikundi ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Ndg Alto Mbikiye amesema kuwa iwapo vitapatikana vikundi vizuri kwa kushirikiana na Maafisa ugani na Maafisa Maendeleo ya Jamii waliopo kwenye maeneo wanatakayofanyia kazi wanaweza kukopeshwa Mitaji ili kutekeleza jambo hilo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa