Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh Innocent Bashungwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo ili wafante shughuli zao katika mazingira rafiki.
Hayo yamesemwa Julai 23 mwaka huu na Mh. Bashungwa wakati akiongea na wafanyabiashara wadogo wa mazao ya mboga mboga na matunda katika eneo wanalofanyia biashara katika kata ya Mtumbatu ambapo amesema wakurugenzi wanapaswa kutenga na kuboresha maeneo ya kufanyia biashara ili wafanyabiashara waweze kuendelea na biashara zao katika maeneo bora na rafiki.
Aidha amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa kuboresha eneo la soko la Mtumbatu kwani wanaweza kufanya biashara masaa 24 kwani eneo hilo limewekwa taa hivyo kulifanya kuwa na mwanga wakati wote hata magari yanapopita usiku wanaendelea kununua bidhaa za wafanyabiashara hao.
Pamoja na hayo ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuendelea kutenga fedha na kutoa mikopo za asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya makundi maalum ili ziweze kuwasaidia kufanya shuguli mbalimbali ikiwemo ujasiliamali kama wafanyabiashara wa soko la Mtumbatu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa