Timu iliyotumwa na Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo kufanya ukaguzi wa Mradi wa Mkaa endelevu Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, unaofanywa na Wananchi kupitia Shirika la TFCG, imejionea mafanikio mbalimbali yaliyotokana na mradi huo.
Licha ya kutoitoa kauli rasmi ya mjumuiko wa ziara hiyo na kudai kuwa Waziri mwenye dhamana ndiye atakaye zungumzia swala hilo lakini pia imewapongeza wananchi wa Kijiji cha Kitunduweta na Ihombwe vilivyopo Kata ya Muhenda kwa mafanikio waliyo yapata kutokana na mradi huo.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi wa TAMISEMI Dr.Charles Mhina pamoja na wataalam mbalimbali wakiwemo Afisa misitu, wataalamu wa Uchumi, wataalamu wa tathmini ya misitu na wengineo, imewapongeza wananchi wa vijiji hivyo kwa mafanikio waliyoyapata sambamba na kuwataka kuendelea na utaratibu wa kuitunza misitu hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wa wananchi wa vijiji hivyo wameshukuru ujio wa mradi huo na kueleza mafanikio waliyoyapata ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa mawili moja Kitunduweta pamoja na nyumba ya walimu hukukijiji cha Ihombwe wakinufaika na kituo cha afya na nyumba ya muuguzi pamoja na kuvuta umeme kituoni hapo na mafanikio binafsi kwa wananchi hao.
Aidha wananchi wameshukuru kuipata elimu ya misitu na kuahidi kuwa watakuwa wasimamizi wazuri katika kuhakikisha inalindwa kwa faida ya Taifa zima.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa