Rai imetolewa kwa Wakuu wa shule na Walimu Wakuu kufuatilia masuala yanayohusu utumishi wa walimu pamoja na kupitisha barua zao, kusimamia maadili ya kazi ya ualimu kwenye maeneo yao,pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu kwa walimu kwa kuzingatia mamlaka yao.
Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) Mathew Kirama katika kikao chake na Wakuu wa shule, Waratibu wa elimu pamoja na Walimu wa wakuu ambapo amesema kuwa Wakuu wa shule wanapaswa kutoa taarifa za utovu wa nidhamu wa walimu kwa mwajiri na kwenye mamlaka ya nidhamu lakini pia amewataka waajiri kuteua Wakuu wa shule na Walimu wakuu wenye uwezo wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
Aidha Kirama amesema kuwaTume ya Utumishi wa Walimu(TSC) inao wajibu wa kushirikiana na waajiri hasa katika ajira, uthibitisho wa mfanyakazi kazini,kupandishwa cheo, kubadilishwa cheo/kazi kwa waliojiendeleza na kutoa taarifa au mrejesho wa masuala ya walimu.
Sambamba na hayo amewataka walimu wote kuwa waadilifu na kutojihusisha na masuala ya kimahusiano ya kimapenzi baina ya walimu na wanafunzi, kutotumikisha wanafunzi katika shughuli zao za nyumbani kam vile kuchota maji lakini pia kutojihusisha na makosa ya kijinai kama vile ugomvi , wizi na ubakaji...
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa