Wakuu wa Shule Wilayani kilosa wametakiwa kuendelea kuhimiza na kuhamasisha Wazazi na Walezi kupeleka Watoto wao shule ili waweze kuandikishwa kujiunga na Elimu ya Awali na Msingi alkadhalika kidato cha kwanza kwa wale waliopangiwa kujiunga katika shule za Umma kwani Elimu ni haki yao ya msingi na ikizingatiwa gharama za masomo zimeshalipiwa na Serikali .
Hayo yamesemwa Januari 8 2024 na Kaimu Afisa Elimu Msingi Richard Mpumilwa ambaye pia ni Afisa Elimu ya watu wazima wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya Shule za Msingi na awali pamoja na Sekondari zilizopo Tarafa ya Kilosa ili kuona mapokeo kwa siku za mwanzo baada ya kufunguliwa shule,kadhalika hali ya uandikishaji na mahudhurio ya Walimu na wanafunzi kwa ujumla wake na kusema kuwa mwitikio katika baadhi ya Shule bado hauridhishi hivyo ipo haja ya kuongeza nguvu katika kuhamasisha wazazi na walezi kuleta wanafunzi shuleni, pia amewataka Wakuu wa shule kuzingatia masuala ya usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu Batuel Ruhega amesema kuwa katika siku ya kwanza ya kufungua shule mahudhurio ya Walimu ni la lazima kwani wao ndiyo wanaoratibu mapokezi ya wanafunzi wanaokuja kujiunga katika shule zao na pia kushawishi Wazazi na Walezi kuleta wanafunzi mapema ili kuanza masomo kwa wakati hivyo amewataka Wakuu wa Shule kusimamia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za kiutumishi katika utendaji wao.
Sambamba na hayo ametoa onyo kwa baadhi ya walimu ambao hawajafika katika vituo vyao vya kazi bila taarifa za maandishi na kwa sababu zisizo na mashiko na kusema kuwa watahesabika kama Watoro, pia amewataka wakuu wa shule kuwa na utaratibu wa kufanya vikao ili kuweza kujadili mambo mbalimbali ikiwemo changamoto zinazowakabili na kuweza kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati.
Naye Katibu msaidizi wa Tume ya Utumishi ya Wlimu Daudi Mchillu amewaasa baadhi ya waalimu kuacha kuchukua mikopo kandamizi kutoka kwenye taasisi ma makampuni ya mikopo kwani hali hiyo inawasababishia madeni hivyo kupelekea utoro kazini ambapo adhabu yake ni kubwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa