Imebainika kuwa mbinu shirikishi baina ya mwanafunzi na mwalimu katika ufundishaji ni njia mojawapo inayoweza kumsaidia mwanafunzi kuwa na uelewa mzuri na kupata matokea chanya hasa katika somo la hisabati.
Hayo yamebainisha na Nelson Kiliba Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Wilaya wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa walimu 52 wa hisabati wa shule za msingi katika tarafa ya Magole wilayani Kilosa kupitia mradi wa hisabati ni maisha ambapo amesema mafunzo ya aina hiyo yatakuwa ni endelevu kwa masomo mengine pia.
Akitoa msisitizo kwa walimu Kiliba amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo katika ufundishaji kwani hisabati inafuata kanuni na kanuni hizo zinapaswa kufuatwa ili kuleta matokeo chanya, hivyo amewataka walimu hao kuzingatia mafunzo hayo na kisha kuyafanyia kazi kinadharia na vitendo pindi wawapo mashuleni.
Aidha Gervas Ndove mkufunzi toka chuo cha ualimu Ilonga wilayani Kilosa ametoa rai kwa walimu hao kuzingatia maneno wanayotumia katika ufundishaji kwani maneno hutegemea aina ya wanafunzi na uelewa wao hivyo ni vema matumizi ya maneno katika ufundishaji yakazingatiwa ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwa haraka na kupata matokeo mazuri.
Na Abrahab Abdul mwalimu toka shule ya msingi Mamboya kwa niaba ya washiriki wenzake amesema mafunzo hayo yametoa mbinu za kumjengea mwanafunzi uelewa kwa ufasaha zaidi na kuwa yatasaidia kupata matokeo mazuri kwa kutumia mazingira waliyonayo wanafunzi na njia mbalimbali za kumfundisha mtoto kwa kumhusisha moja kwa moja.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa