Wananchi wa Kata ya Mtumbatu Wilayani Kilosa wamenufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ikiwemo kliniki ya utoaji wa mikopo ya Asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mikopo ya Wafanyabiashara Ndogondogo Fedha kutoka Serikali kuu ( WBN) kupitia Benki ya NMB, huduma ya bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF), Usajili wa NGOs, Vikundi na Huduma ndogo za Kifedha, Kufungua Akaunti, huduma za kisheria na Maswala ya Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi hilo, Mratibu wa Mikopo ya 10% wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg William J. Mlay amesema kliniki hiyo imeanza rasmi Agosti 17, 2025 na itafanyika katika Tarafa zote Saba Wilayani Kilosa.
"Tumeanza na Tarafa ya Magole katika Kata ya Mtumbatu ambapo tutakuwepo kwa siku mbili na lengo kuu ni kusogeza huduma kwa jamii ili kuwafikia wananchi katika maeneo yao". Alisema Mlay
Mlay ameongeza kuwa wanufanika wa huduma hizo ni wananchi wote wa kata hiyo.
Naye Afisa Dawati la Msaada wa Kisheria Kilosa Ndg. Mladiga Lubele amesema wanatoa ushauri wa Kisheria kwa Wananchi wenye changamoto za kisheria ikiwemo masuala la ardhi, mirathi na kutoa usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala.
Kwa upande wake Afisa Mwandikishaji wa bima iliyoboreshwa CHF, Ndg. Abiney Mhina amewashauri wananchi kujiunga na bima hiyo kwani itawasaidia kupunguza gharama za
hospital ambapo bima hiyo inatolewa kwa watu wasiozidi 6 kwa kaya moja kwa gharama ya Tshs. 30,000/= kwa Mwaka mzima.
Aidha, Bi.Pendo Patrick mkazi wa Kitange kata ya Mtumbatu amesema amepokea vizuri huduma hizo kwani imewarahisishia kupata huduma zote kwa karibu bila gharama yoyote.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa