Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohamed Omary Mchengerwa ametoa wito kwa Wananchi kujikita zaidi katika shughuli za kilimo hususan kilimo biashara ili waweze kujikwamua na hali duni ya kiuchumi na kusema kuwa kazi inayofanywa na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni kubwa hivyo amewataka kutumia fursa hiyo.
Mh Mchengerwa amesema hayo 4,Agosti 2023 wakati alipotembelea viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine amepongeza juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa kiwango ambacho haijawahi kutokea hapo awali.
Amesema kuwa Tanzania imejaaliwa maeneo makubwa na yenye rutuba kwa wingi hivyo haipaswi wananchi wake kukosa chakula na kwamba endapo watu wakijikita katika kilimo cha biashara kila familia itakuwa na uwezo wa kupata mazao ya kutosha kwaajili ya biashara na chakula.
Aidha amewataka Wahesimiwa wakuu wa Wilaya kuhamashisha Wananchi katika maeneo yao kulima kwa wingi kwani kilimo kitaifanya Tanzania kuwa nchi tajiri.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa